Mch. Kiongozi Sosthenes Christopher
Akihubiri kanisani hapo Pastor Sosthenes alisema wakiristo tunatakiwa kujifunza kutokunung'unika mbele za Mungu bali tuendelee kumtukuza kwa kila jambo. kila alieokoka anamahali pake palipo inuliwa na Mungu anakusudia maisha yetu yawe ya mvuto.
Tunapo tii ukweli tutaishi maisha ya mvuto, na wiki yote tumefundishwa kujua ukweli.
Hakuna mtu ambae hataki kuishi maisha mazuri na ndio maana tunahangaika kila siku kwenda makazini, kujishughulisha ili tupate maisha mazuri na ndio makusudi ya Mungu.
Akiendelea, Mch. Sosthenes alikumbusha kuhusu maneno 7 ya kumpa sifa Mungu:
1. Halal : Kusema maneno ya sifa
2. Tehila : Kuziimba sifa
3. Zamar : Kupiga muziki kwa vyombo
4. Yada : Kumuinulia Mungu mikono
5. Shabak: Kutoa heshima kwa sauti kuu
6. Barak : Kumpigia Mungu magoti na kumsujudia
7. Toda : Tendo la shukrani mbele za Mungu kwa sadaka
Mungu ni mwema
ReplyDelete