NGUVU YA SHUKRANI












Ibada ya Juma pili tarehe: 10/11/2013

Akihubiri kanisani LGC, Mch. Sostheness Christopher alisema:

Maana ya shukrani:
Shukrani ni kitendo cha kutambua au kujua matendo ya Mungu katika maisha yetu ya kila siku, maana kila tunachopata maishani mwetu ni kutokana na mapenzi ya mwenyezi Mungu baba yetu.

Ni nguvu inayo sukuma moyo wako kuyashangilia matendo ya Mungu katika maisha yako.

Akifafanua zaidi, Mchungaji Kiongozi Sosthenes alieleza kwamba tunatakiwa kutambua na kumshukuru mwenyezi Mungu katika maisha yetu ili tumpe nafasi ya kuendelea kutenda makuu na mambo ya maajabu zaidi katika maisha yetu.
Zaburi 118: 23

Kwanini tunashukuru ?
1.Jambo njema, Zaburi 92: 1
2.Mapenzi ya Mungu, 1 Wathesanilike 5: 18
3.Ni ufunguo wa kuzipata ahadi za Mungu, Waebrania 10: 36
4.Inakamilisha mzunguko wa maombi, Wafilipi 4: 6
5.Inaleta ongezeko katika maisha yetu, Yohana 6: 5-13, Yeremia 30:19
6.Inafanya yaliokufa kupata uhai tena yohana 11: 41,44

Hatari za Kutokuishi maisha ya shukrani kwa Mungu
1. Yanakukabidhisha kwa adui, kumbukumbu la Torati 28:47-48
2. Yanegeuza maisha yako ya utukufu kuwa aibu, Maisha ya baraka kuwa laana, Malaki 2: 1-3
3. Uharibifu- Maisha yako yanaweza yaharibiwe kama Herode, Matendo ya mitume 12: 21-23



Comments