IBADA YA JUMAPILI 09/03/2014

Pastor Sosthenes Christopher akihudumu

SOMO KUU:
KWANINI TUNAZIHITAJI NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.

1. ILI KUISHI MAISHA YA KUSONGA MBELE.
   Matendo 1:8
-Ukijawa na nguvu hakuna shetani anaweza kuzuia progress yako
  Mithali 4:18
-Ukijawa na nguvu za Mungu mapito yako yataendelelea kung'aa, utasonga mbele kuanzia Yerusalem hata miisho ya nchi.

2. KWA AJILI YA KUHIFADHIWA NA KULINDWA.
- Siwezi kujilinda mwenyewe dhidi ya malango ya kuzimu ni nguvu za Mungu tu juu yangu
   1Petro 1:5
    Luka 10:19

3. KWA AJILI YA MWACHILIO.
   Kutoka 3:19-20
-Israeli walizuiliwa utumwani mpaka nguvu za Mungu zilipozihirishwa wakaachiliwa.
-Zipo nguvu zinazoweza kukuzuia lakini nguvu kuu za Mungu zinapozihirishwa unatoka katika fifungo hivyo.

4.ILI KUYAFURAHIA MATUNDA YA KAZI ZA MIKONO YANGU.
   Isaya 62:8-9
-Si mapenzi ya Mungu taabu ya mikono yangu akala mtu mwingine
  Mhubiri 5:18-19
  Mhubiri 6:2
-Ni karama ya Mungu kufurahia kazi ya mikono yangu na ni Mungu anayeniwezesha kwa nguvu zake kula matunda ya taabu ya kazi yangu.

5.ILIKUPATA MATOKEO HATA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
   Isaya 10:27
   Luka 1:34-35
-Nguvu za Mungu zitafanya yasiyo wezekana yawezekane

HABARI KATIKA PICHA:
Baadhi ya waumini wakifuatilia kwa umakini mahubiri
Baadhi ya waumini wakifuatilia kwa umakini mahubiri

Kwaya ya kina mama LGC wakiwa katika huduma
Praise & Worship Team wakihudumu

 Mchungaji (hayupo pichani) akiongoza maombi

Comments