IBADA YA JUMAPILI 28/9/2014
SOMO: LIFE THAT IS FAR FROM OPPRESSION

THE EFFECTS OF RIGHTEOUSNESS: (MAZAO/MATUNDA YA HAKI)


-There are two types of righteousness
 a)By doing
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. (RUM. 10:5).

  b)By receiving
Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. (RUM. 5:17).
-This disturbed Israelites and many today.
Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. (RUM. 10:3).
Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. (RUM. 10:2).
-After receiving this new kind of life, there are effects.
Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. (RUM. 5:17).
-They that receive...they shall reign in life i.e they shall be kings in life
-To be a king, means you have extraordinary authority.
1. Extraordinary authority.
2. Peace, quietness and assurance forever.
Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. (ISA. 32:17, 18).
-Peace I give unto you...
-Our strength is in...
Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. (ISA. 30:15).
-When...you become unmovable, you will be not shaken in this life; you will be full of assurance.eg father Abraham:
Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi, ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu; (MWA. 14:22, 23).
3. Flourishing and growth.
The righteous shall flourish like the palm tree: he shall grow like a cedar in Lebanon.
Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. (ZAB. 92:12 SUV).
 





SIFA ZA MTENDE.
Mitende mingine hufikia kimo cha meta 30 na huendelea kuzaa matunda kwa miaka 150.
Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. (ZAB. 92:14).
Naam, mtende ni wenye kuvutia na huzaa sana.Gal.5:22-23
 Mtende huzaa mafungu kadhaa ya tende kila mwaka. Fungu moja tu linaweza kuwa na tende 1,000.
Kwa kufaa, Biblia hufananisha watu fulani na mitende.
 Kama mtende wenye kuzaa sana, mtu apaswa kuwa na mwenendo mzuri kiadili na apaswa kuendelea kuzaa matunda mazuri ili kumpendeza Mungu. (Mathayo 7:17-20) Kwa sababu hiyo, michoro ya mitende ilitumiwa kupamba hekalu la Solomoni na pia hekalu ambalo Ezekieli aliona katika njozi. (1 Wafalme 6:29, 32, 35; Ezekieli 40:14-16, 20, 22) Hivyo, ni lazima mtu awe na sifa zenye kupendeza kama mtende ili ibada yake ikubalike kwa Mungu. Neno la Mungu lasema: “Mwenye haki atasitawi kama mtende.”—Zaburi 92:12.
Mwerezi
SIFA ZA MWEREZI WA LEBANONI
1. Unavutia na una thamani kubwa sana.
2. Mrefu sana, unakadiriwa kuwa na urefu kati ya mita 40-45
3. Matawi yake yamesheheni majani
4. Unaishi miaka mingi (approx. 1000-2000 yrs)
5. Unaweza kustahimili misimu yote ( all seasons ) na majani yake hayapukutiki.
6. Una mizizi mirefu sana kwenda chini hivyo haung'oleki kirahisi.
7. Hauozi: kwa sababu hakuna mdudu yeyote anayeweza kuula, una harufu ya asili ambayo hufukuzawadudu wa aina zote.
Sisi tu manukato...
Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu. Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; (2 KOR. 2:14, 15).








Comments