Pastor Emmanuel MbagwileAkihubiri kanisani hapo siku ya kwanza ya semina ya wiki ya shukrani, Mch. Emmanuel alizungumzia kuhusu Nguvu ya shukrani.
Mch. Mbagwile aliye simama kama mhudumu wa kwanza katika wahudumu wa 3 watakao hudumu siku 5 mfululizo katika semina hio alisema:
" Sisi kama wakristo tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kila tendo anaetutendea katika maisha yetu, Na pia kama waumini wa kanisa hili mnatakiwa kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anaewatendea na kuendeleza huduma hii ya LGC maana kila nikija hapa kusema kweli lazima nione mafanyikio na maendeleo."
Akiendelea Mch. Emmanue alielezea maana halisi la neno shukrani kwa lugha ya kihebrania <Todah>
kwamba ni kitendo cha:
Kuungama, Kusifu, Kushukuru, Kuonyesha au kusema asante kewa mtu.
Na kusisitiza kwamba shukrani inaambatana na kitendo cha ukarimu, ndivyo basi, hatuna budi ya kumshukuru mwenyezi mungu kwa matendo yake yote katika maisha yetu.
Zaburi 100:1-4
Mch. Emmanuel alifafanua kwamba, shukrani inaleta matumaini, Nguvu, Baraka na maisha.

Mch. Emmanuel Mbagwile akihubiri
kanisani LGC siku ya kwanza ya semina.
Na kulia ni waumini wa kanisa la LGC wakifuatilia kwa umakini mahubiri.

Comments
Post a Comment