USHUHUDA WA MAMA AGATHA

Hapo pichani ni mama Agatha akiwa anamshukuru mungu na kushuhudia matendo makuu aliemtendea katika ibada ya Ijumaa 15/11/2013.

Akishudia mungu alivyompanya mjukuu wake wa kwanza na ugonjwa wa ajaabu iliotaka kumuondoa maishani baada ya kumpeteza mdogo wake.

" Nilipigiwa sim na mwanangu kwamba mjukuu wangu hali yake sio nzuri kabisa na amelazwa, kusema kweli niliacha shughuli zangu mara mmjoja na kuelekea hospitalini walipo lazwa (Lugalo) na baada ya kufika nikakuta hali ya mjukuu wangu ilikuwa mbaya na hapo hapo nikampigia simu padri maana mi ni mroman(RC) ili aje ambatize mjukuu wangu na gafla baada ya kufanya hivo mjukuu wangu alipoteza maisha. Mara tukapata tena taarifa kuwa mjukuu wangu mwingine aliebaki nyumbani hali yake naye ilibadilika gafla na tukaongozana na mdogo wangu Juliana anaesali LGC kufanya maombi pamoja na Baba mchungaji Sostheness.
 Ndipo Mungu alipo tupigania na kumponya huyu mjukuu wangu aliekuwa anajisaidia tambi za jiko na kumsababishia kuishiwa nguvu.

Pia mimi mwenyewe nilikuwa nasumbuliwa na magonjwa mengi sana zilizonisababishia kuishi na vidonge kwa muda wa miaka 27, nimehangaika katika mahospitali mbalimbali bila kupata nafuu, ila baada ya kufanyiwa maombi na baba Mchungaji nilipata nafuu na hadi leo hii situmii tena vidonge. Ndivyo basi namshukuru Mungu anemtumia Mchungaji Sosthenes pamoja na na kanisa kwa ujumla kwa maombi yenu, mzidi kuniombea pamoja na wanangu ili Mungu atupe nguvu ya kusima kiroho. Na nashukuru sana kwa chakula cha kiroho niliopata hapa LGC."
  


Comments