IBADA YA JUMAPILI 26/01/2014

SOMO KUU:
OFISI SABA ZA ROHO MTAKATIFU/ THE SEVEN DEPARTMENTS OF THE HOLLY SPIRIT
Roho Mtakatifu hufanyakazi kupitia ofisi au idara Saba.
1.Roho wa Uzima (Spirit of life)
2.Roho wa kufanywa wana (Spirit of adoption)
3.Roho wa kweli (Spirit of truth)
4.Roho wa utakatifu (Spirit of Holiness)
5.Roho wa Neema (Spirit of Grace)
6.Roho wa Maombi (Spirit of Supplication)
7.Roho wa Utukufu (Spirit of Grace)

1.ROHO WA UZIMA:
Warumi 8:2,10,11
-Anaihuisha miili yetu na kutupatia Uzima wa Yesu(Yesu ni Uzima Yn 14:6)
-Wakati wa uumbaji Roho wa Uzima alitulia juu ya uso wa maji na Uzima ukaachiliwa
Naomba Roho wa Uzima akatulie juu yako na jambo jema likaziliwe maishani mwako.

2. ROHO WA KUFANYWA WANA (SPIRIT OF ADOPTION)
Warumi 8:15
Katika tamaduni za mashariki adoption ni tofauti na tamaduni za kimagharibi.Walimaanisha mwana aliyezaliwa katika familia na akawa mkomavu na kuwa tayari kulibeba Jina la familia bila kuliaibisha,ndipo babaye humtangaza Kama mwana na kumstahilisha kuwa mrithi wa mali za familia.Wagaratia 4:1-2
-Bwana wetu Yesu alitangazwa na Baba yake-Huyu ni mwanangu mpendwa wangu,msikieni Yeye-Mathayo 3:17 na Mathayo 17:5.
-Tunaambiwa juu yake-...aliendelea katika kimo na hekima akimpendeza Mungu na wanadamu,hii ni Roho wa adoption katika utendaji.
Tunatakiwa kujitiisha na kujinyenyekeza katika uongozi wa Roho Mtakatifu ili atukamilshe na hatimaye tuingie katika urithi wetu wa kutawala pamoja na Kristo.
Yeye hutufunza (He trains us), hutulea(He nurtures us),hutufanya wanafunzi(He disciples us); Hivyo tumruhusu .


Kipindi cha ushuhuda



DADA VUMILIA: 
Huyu dada alikuwa na tatizo la kutokwa na damu mfululizo kwa miezi miwili isivyo kawaida,
Lakini baada ya maombi hapa LGC,Mungu akamponya kabisa na ile hali ya kutokwa na damu mfululizo imekata na sasa ni mzima







IMAKULATA: 
Dada huyu alikuwa na tatizo la kutopata siku zake kwa mwaka mmoja na nusu,baada ya kuombewa aliponywa,ule mzunguko wake wa kila mwezi unaendelea kama kawaida.

















AIMTONGA ABIELI: 
 Huyu mama alikuwa na maumivu makali sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake -Miguu kuota magamba kama nyoka, - Maumivu ya tumbo na kifua; Lakini baada ya kuhudhuria Ibada za maombi LGC,alipona kabisa hadi sasa ni mzima.









THERESIA KALINGA:
 Huyu dada alikuwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu Kila akikohoa,kifua kinawaka kama moto. Lakini alipofanyiwa maombi hapa LGC alipokea uponyaji na hakuna maumivu tena.








Comments