Akihubiri kanisani hapo, Pastor Sosthenes aliendeleza somo kuhusu ofisi 7 za Roho Mtakatifu, na alizungumza juu ya:
ROHO WA KWELI:
Yohana 15:26
Yohana 16:13
Roho wa kweli hutuingiza katika kweli yote.Kwa kadiri tunavyoijua kweli,ndivyo tunapozidi kuingia katika uhuru wetu kwa kuwa imeandikwa utaijua kweli nayo itatuweka huru.Yohana 8:32.
TABIA ZA ROHO WA KWELI:
-Anatufanya tuwe watu tuliojawa na kweli(full of truth;truthful)
-Anatutakasa mbali na kila aina ya uongo(prefabrications,white lies etc)
-Anatutakasa na dhambi zote za ulimi. Katika agano la kale,dhambi za ulimi ni miongoni mwa vitu saba avichukiavyo Mungu.Katika agano jipya tumeamriwa tuishike kweli katika upendo.
-Anatutia nuru tuyaelewe maandiko(He illuminates us)
-Anahuisha na kulifunua Neno kwetu(He inspires and reveals His Word)
- Anatufundisha na kutuongoza(He teaches,corrects and Instructs us)
-Anatukumbusha
-Anatuonyesha mambo yajayo
-Anatushauri nk
Hivyo jenga mazingira ambayo yatamfanya Roho wa kweli ayaguse maisha yako.Tembea katika furaha ya moyo,ruhusu nyimbo ndani ya moyo wako,lazima utamsikia akikuongoza.Isaya 30:29-30.
HABARI KATIKA PICHA
Comments
Post a Comment