IBADA YA JUMAPILI 09/02/2014

Mwendelezo wa somo kuu: Idara saba za Roho mtakatifu
ROHO WA UTAKATIFU:
Warumi 1:3-4.
Yesu Bwana wetu alidhihirishwa kwa uweza kuwa mwana wa Mungu kwa jinsi ya roho ya utakatifu.
-utakatifu sio jambo linaloanzia nje bali ni utendaji kazi wa Roho wa Mungu ndani ya mtu.
-Yesu aliwakemea mafarisayo kwa mkazo wao juu ya mambo ya nje kisha akaelezea umuhimu wa kusafisha ndani na nje hatimaye kunakuwa safi.
-unapookoka,unapokea asili mpya,unakuwa kiumbe kipya,ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya(2Korintho 5:17); tumezaliwa kwa mbegu isiyoharibika kwa Neno la Mungu lidumulo milele(1Petro 1:23);Yesu anafanyika haki kwako na utakatifu (1Korintho 1:30).Asili mpya imeingia ndani mwako.
-Hivyo kwa upya huu wa maisha na kwa kuifuata sheria ya Neno la Uzima
Maisha haya mapya yanajidhihirisha nje.
-Hivyo unapolitenda Neno unasafika zaidi(Zaburi 119:9);Yesu alisema ninyi mmekuwa safi kwa sababu ya lile Neno nililowaambia(Yohana 15:3)
-Utajaribiwa ila Neno litakufanya uwe mshindi(Mwanzo 39:9;42:18)

HABARI MBALIMBALI KATIKA PICHA

Pastor Sosthenes (nyuma), akiombea familia ya Mr. & Mrs. Charles Christopher
katika kutimiza miaka 7 ya ndoa.

Waumini wote wakiwa nashiriki kwenye kuombea familia ya Mr. & Mrs. Charles

Mchungaji akiwaombe baadhi ya waumini baada ya mahubiri
Washirika wakifualitia mafundisho kwa makini
Mama Rose Mhando akitoa matangazo mbalimbali ya kanisa pamoja na kukaribisha wageni waliofika kanisani kwa mara ya kwanza

Timu ya kusifu na kuabudu LGC wakiwa katika huduma

Comments

  1. Ibada ilikuwa nzuri sana, Mungu akubariki Pastor. Ila muandishi aedit kwenye caption ya picha ya mchungaji wakati anafanya maombi, ameandika mcungaji. Mungu awabariki kwa kazi njema.

    ReplyDelete

Post a Comment