IBADA YA JUMAPILI 02/03/2014

5. MEGALEIOTES

Hii ni nguvu kuu ya Roho Mtakatifu iwatoayo wanadamu katika hatma mbaya ambazo adui amewafungia.
Luka 9:43 Neno hili linaonyesha mshangao wa makutano jinsi walivyoona Bwana akiidhihirisha nguvu ya Mungu 'Wote wakashangaa wakiuona ukuu wa Mungu'(And they were all amazed at the migthy power of God-MEGALEIOTES).
- Ni nguvu ya ajabu iwezayo wachukulia watu mizigo ambayo kwa namna ya kawaida isingewezekana.
-Ni nguvu imtoayo mtu toka katika dhambi,toka katika ubinafsi,toka katika mazingira hasi,toka katika mateso nk na kumpeleka mahali pa juu pa maisha ya ushindi.Waefeso 2:6
Kwa nguvu hii ya Roho Mtakatifu naona jinsi Mungu anavyokutoa katika shimo la uharibifu,anavyoitoa Miguu yako toka udongo wa utelezi na kuisimamisha mwambani.
Zaburi 40:1-3.
UBARIKIWE

Mchugaji Sostheness  akiwa anahubiri

Ibada ya kumweka mtoto wakfu



Comments