IBADA YA JUMAPILI 16/3/2014
SOMO: KUBADILISHA VIWANGO KWA NGUVU YA ROHO WA MUNGU.Pastor Sosthenes akihubiri
Tukumbuke kwamba Roho Mtakatifu amekuja
ili tuishi maisha ya kufaa zaidi,maisha ya faida(profitable life),Yn 16:7-Bwana
alisema yawafaa mimi niondoke,maana yake itatufaidia Roho akija.
-Yeye humtoa mtu mavumbini yaani
humbadilishia mtu viwango toka chini kwenda juu.
1Samweli 2:6-8
-Anapokuja juu yako mabadiliko
hutokea,vizuizi huondolewa mbele yako,unapiga hatua moja baada ya nyingine.
Isaya 32:15
-Mungu atakubeba kwa mbawa kama tai
kukupeleka viwango vya juu.
Kutoka 19:4
Mchungaji akiendelea na mahubiri |
JINSI YA KULIFANYA HILI LIWE HALISI
1. KUZALIWA MARA YA PILI
Huu ni mwanzo wa safari ya hatima
njema ya mtu.Bwana alimwambia Nikodemo....hamna budi kuzaliwa mara ya pili-you must be born again-Yohana 3:7
Unapookoka yasiyowezekana
yanawezeka,Mungu anatangulia mbele zako.Isaya 45:1-3.
Kuanzia leo naona Mungu akitangulia
mbele zako!
Mungu anakufanya mzao mteule,taifa
takatifu,mtu wa milki ya Mungu,ukuhani wa kifalme.1Petro 2:9-Ni vema uanze kujiita
Mungu anavyokuita,anza kujiona Mungu anavyokuona.
2.JIONE UNAYO HATIMA NJEMA-SENSE
OF DESTINY.
Kuna mahali kwa ajili yako! Ni
mahali alipo kutengenezea Mungu kwa ajili yako. Kutoka 23:20.
Mawazo yake kwako ni kukupa mwisho
mzuri tena wenye matumaini,kwanini usiwaze hivyo?
Warumi 8:29-30
Yeremia 29;11
Pata picha njema ya mwisho wako huo
kupitia Neno la Mungu na kamwe hutakata tama.
Yesu Bwana wetu alipouona mwisho
wake wa utukufu alidharau aibu na kuustahimili msalaba.Kila unapopata picha
hiyo,utapiga mbio kuelekea hatima hiyo bila kuchoka.Waebrania 12;2-3
Mchungaji akiongoza maombi.
Kipindio cha maombi.
Kwaya ya kina mama ikihudumu.
Comments
Post a Comment