IBADA YA JUMAPILI 6/4/2014

SOMO: NGUVU ILIYOPO KATIKA UTOAJI
Somo hili litatoa maarifa kuhusu:
         -kuwa na mtizamo sahihi kuhusu utoaji
         -kutoa kwa namna iliyo sahihi
         -mahali sahihi pa kutoa
         -aina mbalimbali za utoaji
         -dhawabu za utoaji
         -msukumo katika utoaji
         -nini cha kufanya kati ya utoaji na kuiona dhawabu ya utoaji wako.
          kutoka 25:2

Mchungaji akihubiri katika ibada hiyo
-Mungu anayo sadaka yake.Anasema...mtatwaa kwake sadaka yangu.
-Utoaji ni lango la kuingia katika ulimwengu wa roho. Kama unataka mbingu zako ziwe wazi,kama unataka mbingu zako zizungumze basi utoaji ni jambo lisilo epukika.
-kila mmoja anahitaji msaada toka juu-Zaburi 60;11,utoaji utafungulia msaada huo.
-unapokuwa umeshambuliwa na roho ya uchoyo na ubahili,mahangaiko hayawezi kukuondokea.Bwana alisema jilindeni na choyo-Luka 12:15.
Naona roho hizi zikiachia maisha yako katika jina la Yesu
-katika kila mapato yako,kuna mkate na mbegu.2Korintho 8:10;Kutoka 25:2
-Ni hekima kutambua mbegu katika kila pato lako kwa kuwa mbegu:
         -Itatunza uzao au mtiririko(flow) wa mapato yako
         -Itakuletea mazidisho.Mwanzo 26:12-14
-Hivyo mbegu bora itakuletea matokeo bora.
Kanisa la Makedonia lilijazwa na ukarimu na umaskini haukuwa na nguvu kwao.Ukarimu wao ulijengwa katika misingi mikuu miwili.
1.Walijitoa kwa Mungu
2.Walijitoa kwa watumishi wa Mungu.
kwa kufanya hivi waliweza kutoa kwa uwezo wao na zaidi ya uwezo wao.
NAOMBA NEEMA HII IWE JUU YAKO KATIKA JINA LA YESU.

Habari katika picha




Mzee Katuma akifurahia jambo na watoto wake mara baada ya ibada

Comments